- 18 Jul 2019, 14:10
#19015

Kila mwaka unapofika mwezi wa Muharram, Waislamu wote kwa ujumla na hususan wa madhehebu ya Shia, huomboleza kuuawa shahidi mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Karbala katika mwaka wa 61 Hijria. Hii ilikuwa jihadi kubwa iliyofanywa na Imam Husain kwa ajili ya kuunusuru Uislamu, kwani kama si yeye kujitolea muhanga yeye mwenyewe na kila kitu alichokuwa nacho, leo hii katika Uislamu halali ingekuwa haramu na haramu ingekuwa halali. Ni baada ya Imam kuiona hali hii ndipo alipoamua kupigana jihadi hii kubwa ili kuirudisha heshima ya Uislamu na maadili yake.
Karbala ni ujumbe kwa Waislamu wote kwa ajili ya kusimama kidete kuulinda Uislamu. Imam Husain (a.s.) alijitoa muhanga na akauawa kikatili kwa ajili ya kuitetea dini ya Allah. Hivyo, jukumu letu la sasa na wakati wote ujao ni kuhakikisha kwamba yale aliyofia Imam Husain (a.s.) tunayadumisha, na kwa kufanya kumbukumbu ya tukio hili kila mwaka hutukumbusha jukumu hili na kuleta hamasa kubwa ya kuilinda dini yetu hii ambayo kwa sasa imezungukwa kila upande na maadui wanaouchukia Uislamu. Hivyo, ni juu ya kila Mwislamu kuchukuwa nafasi yake ili kuulinda Uislamu na umoja wake kama alivyofanya Imam Husain (a.s.).
Mwandishi wa kitabu hiki amefanya juhudi kubwa ya kuelezea masaibu haya ya Karbala ili tupate kuzingatia na kutekeleza wajibu wetu katika dini.
Jina la Kitabu : Jihadi ya Imam Husain (a.s)
Mwandishi : Sayyid Muhammad al-Husaini ash-Shirazi
Mtafsiri : Abdul-Karim J. Nkusui
Mchapishaji : Ahlul Bayt (‘a) Centre - Arusha
ISBN :
PDF: https://www.shia-maktab.info/index.php/ ... ad&fid=459

- By BatoolM