Discuss & Debate | Share | Learn

www.ask.or.tz

Our Partners
#18994
Image

Madhehebu ya Ahlul Bayt (a.s.) imetufundisha sisi kwamba Mwenyezi Mungu hana anachofanana nacho. Wake Yeye ni Upweke Kamili, na hakuna viungo au sehemu, hakuna nafasi au mipaka inayoweza kuhusishwa Kwake. Kwa kufanya hivyo, Ahlul Bayt (a.s.) wametupa sisi maana halisi ya Qur’ani Tukufu na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuzing’oa zile fikra zote zisizo sahihi ambazo zilipata kupenyezwa kutoka kwenye kambi za Kiyahudi na Kikristo.

Kinyume na Ahlul Bayt (a.s.), hata hivyo, kuna fikra zilizopo za kusikitisha za kikundi cha wanachuoni wa Kiislamu ambao wamekuwa mawindo ya dhana ya Tawheed isiyo ya Kiislamu. Katika kitabu hiki kuna sura mbili zinazo husu Tawheed, kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Allamah Askari juu ya somo hili, dhana zote zile zenye kumfananisha Mwenyezi Mungu na mwanadamu kwa uzuri kabisa zimekanushwa.

Wanazuoni wa Madhehebu hii wamesimulia kutoka kwa Ahlul Bayt (a.s.), katika vitabu vyao muhimu kama Tafsiir na Hadithi. Matokeo yake, ule muundo asili wa itikadi ya ya Kiislamu umebakia bila kuchafuliwa.

Sasa ni wazi kabisa kwamba, kama isingekuwa kwa juhudi kubwa na bila kuchoka za Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s.) na wafuasi wao, ile imani kuu ya Tawheed ndani ya Uislamu ingeweza kupotea kabisa moja kwa moja.

Jina la Kitabu : Nafasi ya Ahlul Bayt (a.s.) Katika Kuhifadhi Mafundisho ya Uislamu
Mwandishi : Allamah Syed Murtadha Askari
Mtafsiri : Ramadhani Kanju Shemahimbo
Mchapishaji : Al-Itrah Foundation
ISBN : 9987427340

PDF: https://www.shia-maktab.info/index.php/ ... ad&fid=413

Short tafsir on Suratul Faatir (The Originator ) -[…]

Hadith of the day

Imam Sadiq (A.S.)‏ اطْلُبُوا الْعِلْمَ وَ تَز[…]

Today marks the birth anniversary of Imam Hasan al[…]

Hadith of the day

Hazrat Muhammad Mustafa [s] said There are two vi[…]

Ask4help Counseling Helpline