- 31 Dec 2018, 12:48
#18970
Mmoja wa watu mashuhuri na maarufu katika historia ya Uislamu ni Ammar Yasir, Sahaba mtukufu na aliyeheshimika sana wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye aling’aa kama nyota katika ulimwengu wa binadamu katika zama za giza kuu la historia, na akatambulika, kwa sababu ya mng’ao wa nuru ya ukweli, awe kigezo cha kujifunza na kuelimika, na kuwa kielelezo bora cha uhuru na haki.
Ammar ni mmoja katika watu saba wa mwanzo kabisa waliounga mkono harakati tukufu za kueneza Uislamu, na ni mmojawapo wa watu wakubwa kabisa ambao kwamba historia ya binadamu siku zote itajivunia. Siku zote atang’ara katika taji la ubinadamu, kwa sababu alikuwa mmoja wa watendaji wakuu na wafuasi wanyenyekevu wa Uislamu na mmoja wa watumishi watiifu na wajenzi wa historia mpya ya binadamu, na kwa matokeo ya juhudi zake ziendeleazo katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka alipofikia miaka tisini na mbili (92), wakati alipouawa kishahidi katika kutoa huduma kwa upande wa Imam Ali, Kiongozi wa Walioamini. Hakupumzika katika kutafuta na kusema ukweli. Aliifurahia sana nafasi hiyo yenye kufanikiwa ambayo kwamba mtu asiyeweza kulinganishwa na mwingine, yaani Ali, alitoa machozi wakati anamwomboleza, alisoma kisomo cha maombolezo chenye kuhuzunisha sana, alipotenganishwa naye, na alimwomba Mungu kuhusiana na kifo cha kishahidi cha Sahaba huyu mkubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
Jina la Kitabu : Ammar Yasir : Msahaba Mjulikana wa Mtukufu Mtume (saww)
Mwandishi : Sadruddin Sharafuddin
Mtafsiri : Mganga B. Mnuve
Mchapishaji : Al-Itrah Foundation
ISBN : 9987427170
PDF: https://www.shia-maktab.info/index.php/ ... ad&fid=388